Ijumaa 18 Aprili 2025 - 09:53
Ghaza haitashindwa kamwe

Ayatollah al-Jawahiri amesisitiza “nafasi isiyo na mfano ya maulamaa katika kuilinda Umma”, ameuita ushindi wa Gaza kuwa hauepukiki, na aina yoyote ya kujisalimisha mbele ya adui ni khiyana kwa malengo ya Imam Hussein (a.s).

Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza", Ayatollah Hassan al-Jawahiri, mwanazuoni mashuhuri wa kidini na mwalimu katika Hawza ya Najafu Ashraf, amesisitiza umuhimu wa nafasi ya maulamaa katika kuongoza Umma na kukabiliana na changamoto za zama hizi, na akaongeza kwa kusema: “Uongozi wa kidini huko Najafu umejifunga kwenye njia ya uadilifu, hekima, na kutumia akili.”

Akinukuu munājāt (dua za faragha) za Imam Ali (a.s) katika mwezi wa Sha‘ban, mewataka waislamu kumuelekea ya Mwenyezi Mungu na kumtii, na akatoa onyo kwamba neema za Mwenyezi Mungu hazipaswi kupuuzwa kwa kumuasi, na akaliita tendo hilo kuwa ni “tendo ovu kubwa.”

Mwalimu wa Hawza ya Najafu aliita madai ya ushindi wa Israel huko Ghaza kuwa ni “dhana”, na akasisitiza: “Ghaza haijawahi kushindwa kamwe, na hata siku zijazo haitashindwa.”

Ulama huyo ametoa onyo kuwa wito wa kujisalimisha mbele ya adui ni kinyume na njia ya Imam Hussein (a.s), na akasema: “Hawza zimesimama pamoja na wanyonge wa Ghaza, Lebanon, na maeneo mengine.”

Ayatollah al-Jawahiri alilitetea dhana ya “Wilāyat al-Faqīh” na akaiona kuwa ni muendelezo wa uongozi wa Mtume (s.a.w) na Maimamu (a.s) katika kuongoza mambo ya Umma.

Kisha akaendelea kusema: “Kuwasaidia wanyonge ni jukumu la kisheria, na ukimya wa baadhi ya serikali mbele ya jinai za wavamizi ni ‘khiyana kwa malengo ya Kiislamu.’”

Ayatollah Al-Jawahiri alihitimisha hotuba yake kwa kusisitiza tena kwamba jihad na muqawama vinaendelea, na akaashiria nafasi ya kihistoria ya maulamaa, na akawaomba waislamu wawe na makini mbele ya uvamizi wa fikra na utamaduni wa magharibi dhidi ya maadili ya Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha